Tuesday, October 29, 2013

MWANAFUNZI AJIUA KUONDOKA NA AIBU

MWANAFUNZI wa Darasa la tano Katika Shule ya Msingi Kitanda katika halmashauri ya wilaya ya Tunduru aliyefahamika kwa jina la Faudhia Suleiman Ally Kawalula (14) amejinyonga hadi kufa kwa madai ya kuondokana na aibu ya tukio la Wizi.

Mashuhuda wa Tukio hilo walisema kuwa Mwanafunzi huyo alikutwa akiwa aejinyoga kwa kutumia kamba asubuhi ya kuamkia oktoba 27 mwaka huu nda ya chumba alicho kuwa akilala nyumbani kwao.

Wakizungumzia chanzo cha tukio hilo kwa masharti ya kutotajwa majina yao gazetini miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa kabla ya mwanafunzi huyo kuchukua maamuzi hayo alituhumiwa kuiba Tsh. 5000 kwa muuza duka jirani na nyumba yao .

Walisema baada ya tukio hilo ambalo lilidaiwa kufanyika kwa ustadi mkubwa na alipo guindulia tayali akuwa amekwisha nunua nguo za ndani, mafuta ya kupaka na sabuni vitu ambavyo muuza duka huyo alivitaka
apewe ili aviuze kwa ajili ya kufidia fedha yake hali ambayo ilimuweka binti huyo katika aibu na kumfanya achukue hatua hiyo.


Akizungumziaa tukio hilo Baba mzazi wa marehemu  Suleiman Ally Kawalula alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo mbali na kuithibitisha kuwepo kwa tukio la kifo hichi alidai kuwa hakuwa na taarifa zozote juu ya tukio la wizi huo kwa madai kuwa yeye alikuwa akiishi kwa mkewe wa pili katika eneo la kijiji cha azimio.

Nae kaimu mtendaji wa kijiji hicho hashim Mpunga alisema kuwa baada ya kupokea taarifa za tukio hilo kutoka kwa wasamalia wema alipeleka taarifa kituo cha polisi haraka kwa ajili ya kuomba msaada wa wataalamu wa kitabibu ili kutoka nafasi kwa wanafamilia kufanya maziko ya mpendwa wao.

Mganga aliyefanya uchunguzi wa mwili wa marehemu Faudhia, dkt. Titus tumbu alisema kuwa chanzao cha kifo hicho kilitokana na marehemu kujifunga kwa kamba Shingoni na kujibana kooni na kumfanya kukosa hewa kwa muda mrefu.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma deusdedit Nsemeki amedhibitisha kuwepo kwa tukio hilo alisema kuwa Polisi bado wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kujiridhisha kama kweli alijinyonga au la.

No comments:

Post a Comment